FARAGHA
Sera ya Faragha
Jinsi MONTANA STORE inavyokusanya, kutumia na kulinda taarifa zako.
Taarifa tunazokusanya
Unapoagiza tunahifadhi jina, namba ya simu, mkoa, wilaya, anwani, bidhaa ulizoagiza na taarifa za malipo (mtandao, namba ya kulipia, kiasi na kumbukumbu ya muamala). Ukituma fomu ya mawasiliano tunahifadhi jina, email, simu na ujumbe wako.
Matumizi ya taarifa
Taarifa hizi hutumika kushughulikia oda, kuthibitisha malipo, kufikisha mzigo na kuwasiliana nawe. Hatuuzi taarifa zako kwa mtu yeyote.
Malipo
Malipo yanashughulikiwa na mtoa huduma wa malipo. Hatuoni wala kuhifadhi PIN yako.
Kikapu na kifaa chako
Bidhaa za kikapu na mazungumzo ya msaidizi huhifadhiwa kwenye kivinjari chako tu.
Mawasiliano
Kwa maswali kuhusu taarifa zako, tumia ukurasa wa Wasiliana Nasi.